Hong Kong yatakiwa kujali Demokrasia

Haki miliki ya picha Getty
Image caption waandamanaji china

Marekani kwa mara nyingine imeitaka Hong Kong kuzingatia demokrasia kamili kutokana na maandamano yanayoendelea kushinikiza serikali ya nchi hiyo kuzingatia maoni ya wananchi.

Hata hivyo Raia wa Hong Kong wametakiwa kuunga mkono mapendekezo ya serikali kuhusiana na mabadiliko ya mfumo wa serikali.

Mkurugenzi wa eneo hilo C.Y. Leung amesema kuwa ni matumaini yake kwamba pamoja na maandamano yanayoendelea nchini humo lakini bado idara zote zitaendelea kufanya kazi zake kama kawaida..

Maelfu ya waandamanaji wapo mitaani wakipinga mpango wa serikali ya China kuhusiana na kupitisha jina la mgombea badala ya Leung katika uchaguzi wa 2017.

Hata hivyo Marekani kwa mara nyingine imeitaka China kuzingatia demokrasia kamili.

Idara za serikali nchini humo zinasisitiza kuwa mtendaji mkuu ni lazima achaguliwa kwa mapendekezo ya wananchi.