Vitisho vya wanafunzi wa Hong Kong

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Wanafunzi wametishia kuvamia majengo ya serikali ikiwa kiongozi wa Hong Kong hatajiuzulu

Wanafunzi kati eneo la Hong Kong wameahidi kuendeleza maandamano iwapo mkuu wa utawala katika eneo hilo CY Leung hataachia madaraka.

Kiongozi wa wanafunzi hao Lester Shum amesema kwa sasa wana mpango wa kuanza kuyazingira majengo ya serikali kama kiongozi huyo hatajiuzulu hadi alhamisi wiki hii.

Kwa maelfu ya watu wameendelea kusambaa katika mitaa mbalimbali ya Hong Kong.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Ofisi nyingi zitasalia kufungwa hadi Alhamisi kwa sababu ya likizo ya kitaifa

Hata hivyo kiongozi wa wanafunzi hao amesema kuwa ni matumaini yao kuwa kiongozi huyo atajiuzulu kati leo ama Alhamisi.

Maelfu ya watu bado wanaandamana na kuendelea kukita kambi katika mji na maeneo mengine ya makutano katika eneo hilo.

Ofisi katika mji huo zitafungwa hadi keso kwa sababu ya likizo kuadhimisha siku ya kitaifa nchini China.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Wanafunzi ndio wengi zaidi walioshiriki katika maandamano haya

Bwana Leung alitopa hotuab tyake kuwataka wananchikukubali sheria mpya za uchaguzi hali ambayo ilizua maandamano hayo.

Alisema kuwa wagombea wote watapata tiketi ya moja kwa moja ya uchaguzi kuanzia mwaka 2017.