Wanawake na siasa Tunisia

Haki miliki ya picha BBC World Service

Wanawake nchini Tunisia wameendelea kupigania haki zao ili kushika nyadhifa za kisiasa kwa mjibu wa katiba ya nchi hiyo,hata hivyo baadhi ya wanawake wameanza kuonyesha wazi wazi jitihada za kujikomboa kiuongozi.

Katika hali ambayo haikuwepo siku za awali nchini humo kwa sasa baadhi ya wanawake wanahudhuria mafunzo ya wazi yanayowapa mbinu za kuwa wanasiasa wenye ushindani dhidi ya wanaume.

Kama ambavyo walionekana baadhi ya wanawake wakiwa wamekaa mbele ya mti huku wakiandika baadhi ya dondoo mhimu katika mafunzo yanayotolewa na taasisi moja isiyo ya kiserikali kuhusiana na mafunzo ya kisiasa kwa wanawake hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa nchi hiyo.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Wanawake katika warsha ambako wanajfunzwa kujiamini na kujithamini katika ulingo wa siasa

“Wanawake nchini Tunisia wanatakiwa kujengwa katika kujiamini ili waweze kufikia hatua ya kushika vyeo vya kisiasa”anasema mwezeshaji mafunzo ya kisiasa kwa wanawake kutoka asasi isiyokuwa ya kiserikali ambayo imekuwa ikitoa mafunzo ya kuwapa ujasiri na mbinu za kisiasa wanawake ili waweze kugombea nyadhifa mbalimbali.

Katika kipindi ambacho wanawake wa nchi za kiarabu wanapigania haki zao, hali imekuwa tofauti nchini Tunisia ambako wanawake kwa uwazi kabisa wamefikia hatua ya kuelezea haki zao hadharani kushinikiza utekelezwaji wa katiba mpya iliyopitishwa mwaka huu inayosisitiza umhimu wa kuwa na wanawake katika vyeo vya kisiasa.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Wanawake wana historia ndefu katika harakati za kutetea haki zao nchini Tunisia

Hata hivyo wanawake hao wanasema kuwa maneno matupu iwapo haki ya wao kushiriki katika siasa haitatekelezwa katika uchaguzi mkuu wa mwezi ujao mwaka huu.

Lebna Jeribi ni mbunge kutoka chama cha Ettakatol yeye anasema jambo la kuzingatia ni sheria tu na kuvishinikiza vyama vya siasa kuwafikia wanawake ili waweze kuwania uongozi.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Wanawake wabunge wa chama tawala wanahisi wamekuwa katika msitari wa mbele kutetea katiba nzuri

Sheria ya uchaguzi nchini Tunisia inaeleza kuwa katika majimbo yote ya uchaguzi 33 ni lazima kuwe na usawa kati ya wanawake na wanaume,hadi sasa kuelekea uchaguzi mkuu ujao ni aslimia 11.2 tu ya wanawake ndiyo waliopo katika orodha ya wanaowania uchaguzi huo.

Wanawake nchini Tunisia wana historia ndefu ya kudai ukombozi wao katika kushiriki kushika nyadhifa za kisiasa kama ambavyo maandamano ya Ennahda yaliyofanyika mwakajana.