Ebola:Hofu kwa watoto Marekani

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Liberia ndio moja ya nchi zilizoathirika vibaya sana kutokana na Ebola

Watoto watano katika jimbo la Texas nchini Marekani waliokutana na mwanamume anayeugua Ebola nchini humo, wanachunguzwa kwa karibu nyumbani kubaini ikiwa wana dalili zozote za ugonjwa huo.

Kwenye mkutano na wandishi wa habari katika hospitali ya Texas Health Presbyterian mjini Dallas, gavana wa jimbo hilo alisema kuwa wazazi wa watoto hao wana wasiwasi lakini aliwahakikishia kuwa hakuna tisho la maambukizi.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Zaidi ya watu 3,000 wamefariki kutokana na Ebola katika kanda ya Afrika Magharibi

Maafisa wamesema kuwa watoto hao wanachunguzwa kwa karibu na nkwamba kuna wanawachunguza watu wengine 12 au zaidi ambao huenda walikaribiana na mwanamume anayeugua Ebola.

Mgonjwa huyo Thomas Duncan anaaminika kuambukizwa Ebola alipokuwa nchini Liberia.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Duncan ni mgonjwa wa kwanza wa Ebola kupatikana nchini Marekani

Raia huyo wa Liberia aliingia nchini Marekani wiki mbili zilizopita kuwatembelea jamaa wake, na ni mtu wa kwanza kugunduliwa na Ebola akiwa nchini Marekani.

Bwana Duncan yuko katika hali mbaya kwa mujibu wa wahudum,u wa afya wanamuhudumia.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Kwa sasa yuko katika hali mbaya katika hospitali ya Texas Health Presbyterian

Muuguzi alimuuliza bwana Duncan alipotembelea hospitali lini alianza kujihisi mgonjwa na ikiwaaliwahi kuwepo katika eneo lililoathirika na Ebola.

Alimwambia kuwa alikuwa ametembelea Liberia, lakini taarifa aliyokuwa anatoa hakuwa ameitoa kwa kikosi kizima kilichohusika na matibabu yake hospitalini.