Punda wapendanao wazua kihoja

Image caption Punda hawa walizua kihoja kutokana na tabia yao ya kujamiiana mara kwa mara

Punda wawili wanaopenda kucheza pamoja na kujamiiana sana wameunganishwa tena nchini Poland.

Wawili hao kwa majina Antonina na Napoleon wanadaiwa kupendana kwa miaka 10,lakini walitenganishwa na wafanyakazi katika hifadhi moja ya wanyama ya Poznan nchini Poland baada ya malalamishi kwamba mienendo yao ya kujamiiana kila wakati huenda ikawapotosha watoto.

Swala hilo lilizua mjadala mkubwa nchini Poland huku wanasiasa na watu maarufu wakijaribu kuipima hatua hiyo. Taarifa hii ni kwa mujibu wa mtandao wa Daily Nation

Stefan Niesiolowski wa chama tawala cha Civic Platform amesema kuwa ni upuzi mkubwa kuwatenganisha wanayama hao katika maeneo tofauti eti kwa kuwa wanapendana sana.

Hata hivyo pendekezo la kuwaunganisha wapenzi hao wawili liliungwa mkono kwa kupata saini 7000,na sasa eneo hilo la kuhifadhi wanyama limebatilisha uamuzi wake kwamba Punda hao ambao wanaweza kuishi kwa pamoja.