Liberia kumshitaki mgonjwa wa Ebola

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Duncan ni mgonjwa wa kwanza kugundulika na Ebola nchini Marekani

Maafisa wa utwaala nchini Liberia, wanasema kuwa watamshitaki mwanamume aliyepatikana na ugonjwa wa Ebola nchini Marekani wakimtuhumu kuwa alitoa taarifa za uongo kuhusu kukutana na jamaa wake aliyekuwa anaugua ugonjwa huo.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Wasafiri wanakaguliwa na kuulizwa maswali kabla ya kusafiri kutoka Liberia

Mgonjwa huyo Thomas Eric Duncan alitakiwa kujibu maswali kadhaa kabla ya kusafiri kwenda Marekani mwezi jana lakini maafisa wanasema aliulizwa ikiwa alikutana na jamaa yake mwenye virusi hiyo akasema la. Alisema hakuna jamaa yajke yeyote anaugua ugonjw ahuo.

Lakini waziri wa afya amesema kuwa mwanamume huyo alionekana akimpeleka jamaa wake mgonjwa hospitalini.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Liberia ni moja ya nchi zenye idadi kubwa ya wagonjwa wa Ebola katika kanda ya Afrika Magharibi

Bwana Duncan yuko katika hali mahututi, katika hospitali ya Dallas.

Ni mgonjwa wa kwanza wa Ebola kugudnulika nchini Marekani ambako zaidi ya watu 100 wanachunguzwa ikiwa wameambukizwa ugonjwa huo.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Ni maafisa wa afya pekee wanaoruhusiwa kuwachukua wagonjwa kutoka majumbani kwao

Zaidi ya watu 3,330 wamefariki kutokana na Ebola katika nchi nne za kanda ya Afrika Magharibi.

Taarifa ya kutaka kumfungulia mashitaka mghonjwa huyo ilitolewa katika mkutano wa kila wiki wa serikali kuarifu waandishi wa habari kuhusu hali ya ugonjwa huo nchini humo.