USA:Yaunga mkono ukaguzi wa Ebola

Image caption Ukaguzi wa ebola katika uwanja wa ndege

Maafisa wa usalama jijini Washington wanasema kuwa wana imani kuwa ukaguzi wa kiafya kwenye viwanja vya ndege Magharibi mwa Afrika utazuia watu wengi walio na ugonjwa wa Ebola kuelekea nchini Marekani.

Mshauri mmoja katika ikulu ya white House Lisa Monaco amekataa wito wa kutaka kuwekwa kwa marufuku ya usafari kutoka magharibi mwa Afrika akisema kuwa hatua kama hizo zitaambulia patupu.

Mwanamme mmoja kutoka Liberia aliyepatikana na ugonjwa wa Ebola akiwa nchini Marekani sasa anapata matibabu kwenye hospitali moja kwenye jimbo la Texas.

Marekani imesema kuwa itatuma hadi wanajeshi 4000 kwenda Magharibi mwa Afrika kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola ambao umesababisha vifo vya hadi watu 3,500.