Dewani mahakani kwa kifo cha mkewe

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Familia za Shrien na Anni Dewani

Familia ya Anni Dewani mwanamke aliyeuawa nchini Afrika Kusini akiwa kwenye fungate karibu miaka minne iliyopita, inasema kuwa inataka ukweli.

Shrien Dewani anafikishwa mahakani kwa kumuuaa Anni ambaye baada ya kuoana kwa wiki mbili tu.

Analaumiwa kwa kupanga mauaji yake . Bwana Dewani ambaye anatokea Bristol alipoteza kesi yake ya miaka mitatu ya kupinga kurudishwa afrika kusini mwezi Aprili baada ya kuchukua muda mwingi akipata matibu ya shinikizo la mawazo baada ya mauaji hayo.

Kati ya maswali yanayoulizwa ni pamoja na ikiwa bwana Dewani alipanga njama ya kumuua mwanamke ambaye walikuwa wameoana kwa wiki mbili tu au ni mbinu ya afrika kusini ya kutaka kuficha ukweli kuhusu kuongezeka kwa visa vya uhalifu nchini mwake.

Familia zote zinatarajiwa kuhudhuria kesi hiyo. Wanaume watatu ambao wamefungwa kwa kuhusika na mauaji hayo wanadai kuwa Shrien Dewani ndiye aliyapanga na wanatarajiwa kutoa ushahidi wao mahakani.

Lakini bwana Dewani anatarajiwa kuieleza mahakama kuwa yeye pamoja na mkewe Anni walikuwa ni waathiriwa wa utekaji nyara na uvamizi kwa watalii ambao Afrika Kusini inataka kukataa.

Ashok Hindocha ambaye ni mpwa wake Anni anasema kuwa familia yao imejiandaa kwa siku ngumu za usoni lakini kile wanachotaka ni ukweli.