Abakwa akimtembeza Mbwa

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Mwanamume aliyetenda uovu huo anasakwa na polisi nchini Uingereza

Mmanamke mwenye umri wa miaka 40 amebakwa akiwa anamtembeza Mbwa wake katika mtaa wa Salford nchini Uingereza.

Alikuwa anatembea karibu na jumba la New Bank Towers siku ya Jumapili alipokutana na mwanamume mmoja ambaye hakumfahamu ila wlaitembea pamoja.

Walipowasili naye katika barabara ya Mount, alisukumwa kichakani na kubakwa na mwanamume huyo.

Inaarifiwa mwanamume huyo anayesakwa na polisi, alimhadaa mwanamke huyo na kisha kumsukuma kichakani kabla ya kumtendea uovu huo.

Maafisa wa polisi, wanasema kuwa kitendo hicho kilikuwa kibaya sana na kwamba wanafanya uchunguzi.