Wapigwa na radi wakiomba nchini Colombia

Image caption Nyumba walimokuwa wanafanyia mambo watu wa Wawi iliteketea yote

Watu saba wa jamii moja nchini Colombia wamefariki baada ya kupigwa na radi wakiwa katika shughuli ya maombi katika eneo moja milimani Kaskazini mwa nchi hiyo.

Viongozi kutoka kabila la Wiwa walikuwa wanafanya maombi walipopigwa na radi.

Watu wengine 15 walijeruhiwa.

Walionusurika waliokolewa na jeshi na kupelekwa hospitalini mjini Santa Marta.

Wengi wa walioathiriwa wanapokea matibabu baada ya kupata majeraha mabaya.

'madhabahu yateketea'

Mkasa huo ulitokea Jumapili usiku karibu na mji wa Guachaca, katika milima ya Sierra Nevada.

Takriban watu 60 walikuwa wamekusanyika kwa sherehe maalum ya maombi, ndani ya nyumba ndogo ya nyasi wakati ilipopigwa na radi.

Nyumba hiyo iliteketea yote.

''Tunawaombea watu wa jamii ya Sierra Nevada,'' alisema Rais Juan Manuel Santos kwenye akauti yake ya Tiwtter.