Michezo:Hofu ya dawa kutoisha mwilini

Haki miliki ya picha Getty
Image caption justin_gatlin

Wanariadha waliofungiwa kutokana na kutumia dawa za kusisimua misuli kama Justin Gatlin, wanaweza kunufaika na dawa hizo hata baada ya muda waliofungiwa kumalizika kwa kipindi cha miongo kadhaa.

Utafiti uliofanywa na wanasayansi wa chuo kikuu cha Oslo umeonyesha kuwa misuli inaweza kuhifadhi dawa hizo kwa miongo kadhaa tangu mwanariadha alipoanza kuzitumia.

Gatlin mwenye umri wa miaka 32 alikimbia kwa kasi isiyo kawaida kwa mtu mwenye umri kama wake katika mbio za mita 100 na 200 hali inayoonyesha kuwa dawa hizo bado zina nguvu mwilini mwake licha ya kufungiwa mara mbili kutoshiriki mbio hizo.