Al Shabab waondoka Barawe

Haki miliki ya picha AP
Image caption Al Shabab

Majeshi ya Somalia na Umoja wa Afrika AU yamesema kuwa yamefanikiwa kuikomboa bandari iliyokuwa ikishikiliwa na makundi ya wapiganaji wa kiislam.

Milio ya risasi ilisikika kadri majeshi ya serikali ya Somalia na AU yalipoingia Barawe mji uliopo kilomita 220 kusini Magharibi mwa mwa mji mkuu wa Somalia Mogadishu.

Umoja wa mataifa umesema kuwa wapiganaji hao wa Al shabaab waliweka ngome katika eneo la Barawe ili kufanya mashambulizi mji mkuu wa nchi hiyo Mogadishu.

Mara ya mwisho kwa Somalia kushikilia mji huo ilikuwa miaka 23 iliyopita.

Majeshi ya AU yamekuwa yakishirikiana na majeshi ya serikali ya Somalia kukabiliana na wapiganaji wa Al Shabab,hata hivyo baadhi ya raia wa eneo hilo wanasema kuwa wapiganaji wa Al shabab walianza kuondoka katika eneo hilo tangu ijumaa wiki iliyopita.