Jules Bianchi afanyiwa upasuaji

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Jules Bianchi

Familia ya Jules Bianchi dereva wa magari maarufu ya langa langa imeelezea hatua za matibabu ya ndugu yao anayoyapata kufuatia ajali aliyoipata iliyomsababishia majeraha kichwani kwake. Bianchi amefanyiwa upasuaji siku ya jumapili na hali yake inaelezwa kuwa nzuri japo kuwa bado yupo katika chumba cha wagonjwa mahututi.

Shirikisho la mchezo huo limemtaka mkurugenzi wa mashindano hayo ya langa langa Charlie Whiting kutoa maelezo kamili kuhusiana na chanzo cha ajali hiyo.

Wanafamilia hao wamekielezea kipindi hiki kuwa ni kigumu kwao kutokana na nafasi ya Bianchi katika familia yao na kwamba amekuwa msaada sana kwao.