Kiazi chamea ndani ya kizazi

Haki miliki ya picha Thinkstock
Image caption potatoes

Kiazi kilipatikana kikimea ndani ya kizazi cha mwili wa mwanamke mmoja baada ya kujaribu kukitumia kama kifaa cha kuzuia mimba.

Msichana huyo mwenye umri wa miaka 22 kutoka nchini Colombia ambaye jina lake halikutajwa alijaribu kutumia kiazi hicho ili kuzuia mimba na alipomtembelea daktari baada ya kulalamika kuhusu maumivu ya tumbo ,iligunduliwa kuwa kiazi hicho kilikuwa kimeota mizizi ambayo ilianza kumea ndani ya kizazi chake.

Kulingana na Gazeti la Nation nchini kenya msichana huyo amedai kuwa mamaake alimshauri kwamba iwapo angependelea kuzuia mimba basi alifaa kuweka kiazi ndani ya kizazi chake.

Licha ya hatari aliyokumbana nayo mwanamke huyo hakuathirika huku kiazi hicho kikitolewa bila kufanyiwa upasuaji.