Marekani ina kibarua kigumu Syria

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wanajeshi wa muungano kutoka mataifa washirika wanakabiliana na wapiganaji wa IS Syria

Wizara ya ulinzi ya Marekani imesema inafanya kila iwezalo kuzuia wapiganaji wa ISIL kuudhibiti mji wa Syria Kobane.

Lakini mwenyekiti wa wakuu wa jeshi la pamoja, Jenerali Martin Dempsey, amesema wanamgambo hao wamekuwa wakijifunza jinsi ya kukwepa makombora ya angani.

Jeshi la Marekani linasema linaamini Wakurdi bado wanadhibiti sehemu kubwa za mji huo licha ya kushambuliwa pakubwa hapo jana.

Ufaransa imeunga mkono pendekezo la Uturuki kuunda eneo litakalodhibitiwa kiusalama katika mpaka wake na Syria ili kujilinda na pia kuwasaidia wakimbizi wa Syria.

Jenerali mstaafu Wesley Clark awali aliyehudumu kama kamanda wa juu wa jumuiya ya kujihami NATO kwa Ulaya, amesema ana imani kwamba operesheni dhidi ya IS hatimaye itafaulu.