EU kuzuia wapiganaji wa kigeni

Haki miliki ya picha FARS
Image caption Wapiganaji wengi wa kigeni wamekuwa wakienda kupigana nchini Syria na Iraq

Mawaziri wa mambo ya ndani wa Umoja wa Ulaya wanakutana mjini Luxembourg leo kujadili njia za kusitisha raia wa Ulaya waliopigana Syria kurudi na kufanya mashambulio ya kigaidi katika nchi wanazotoka.

Inakadiriwa kwamba raia wapatao 3000 wa Ulaya wamesafiri kwenda Syria.

Mipango kadhaa inajadiliwa kujaribu kutoa ulinzi bora zaidi dhidi ya mashambulio ya kigaidi.

Moja ni data ya wasafiri wa ndege kwa Ulaya ambayo itasaidia kuwatambua na kuwasaka washukiwa wa ugaidi.

Wabunge wa bunge la Ulaya tayari wamepiga kura kupinga pendekezo moja hatahivyo wakilalamika kwamba uangalizi wa mamilioni ya wasafiri utakuwa ni ukiukaji wa uhuru wa raia.

Mawaziri pia wanataka kusitisha mitandao ya kijamii kutumika kama chombo cha usajili kwa makundi yenye itikadi kali za dini ya kiislamu.

Hapo jana usiku wakurugenzi wa mitandao ya Google, Facebook na Twitter walikutana na maafisa wa serikali kubaini vipi wanavyokabiliana na itikadi kali katika mitandao.