Mwanajeshi wa kwanza wa UN afariki CAR

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wanajeshi wa Umoja wa mataifa nchini CAR

Mwanajeshi mmoja wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa amekuwa afisa wa kwanza wa kuweka amani kufariki nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati baada ya walinzi wa msafara wao kushambuliwa nje ya mji wa Bangui.

Kulingana na maafisa, mwanajeshi huyo wa Pakistani aliuawa katika ajali ya barabarani wakati gari la wanajeshi wa Umoja wa Mataifa liliposhambuliwa usiku wa kuamkia alhamisi.

Vilevile wanajeshi wengine wanane walijeruhiwa huku mmoja wao akipata majeraha mabaya.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kundi la wapiganaji wa CAR

Takriban watu 5,000 wameaga dunia kufuatia machafuko ya kidini nchini Jamhuri ya afrika ya kati.

Mapigano mapya yalizuka wiki hii - yakiwa ni mabaya zaidi tangu Umoja wa Mataifa kuchukua usukani wa kulinda amani mwezi Septemba.

Milio ya risasi ilisikika katika mji mkuu siku ya Alhamisi.

Mwandishi wa BBC aliye mjini Bangui, anasema kuwa hakuna watu barabarani huku vituo vya mafuta, maduka na mashirika ya kibinadamu yakifungwa huku wafanyikazi wa mashirika ya kibinaadamu wakiagizwa kusdalai majumbani..