Uturuki kuzuia ndege kutumia anga lake

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption mapigano

Waziri wa masuala ya kigeni wa Uturuki Mevlut Cavusoglu amesema hawategemei kuongoza mashambulizi ya ardhini katika operesheni dhidi kundi la wapiganaji wa Kiislam IS.

Cavusoglu amesema kuwa nchi yake inampango kuzuia ndege kutumia anga lake lililopo katika eneo la mpaka wake na na Syria ikiwa ni matokeo ya mazungumzo waliyoyafanya na mkuu wa majeshi ya NATO Jens Stoltenberg.

Uturuki imekuwa katika harakati za kuwasaidia wapiganaji wa Kikurdi wanaopigana na kundi la wapiganaji wa Kiislam la IS ambao wanawania kuuchukua mji wa Kobane.

Hata hivyo makundi ya uchunguzi kutoka Syria mapema yalikaririwa yakidai kuwa wapiganaji wa IS wanashikilia robo tatu ya mji wa Kobane

Saa chache zilizopita wingu la moshi mkubwa lilitanda angani katika kilele cha mlima wa mji wa Mistanour kutokana na mapigano yanayoendelea.