Raia 700 wakwama mjini Kobane, Syria

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Steffan de Mistura

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Syria ameonya kuwa hadi watu 700 wengi wao wakiwa watu wazima wanaendelea kukwama katika mji wa mpakani mwa Syria Kobane.

Staffan de Mistura pia ameitaka Uturuki kuruhusu watu waliojitolea nchini Syria kuutetea mji huo kutoka kwa wapiganaji wa Islamic State.

Kuna ripoti kwamba Islamic state imechukua udhibiti wa makao makuu ya kikurdi katika mji huo lakini madai hayo yamekanushwa naa afisa mmoja wa kikurdi.

Kobane limekuwa eneo la mapigano kati ya wanamgambo wa Islamic State na wale wa kikurdi.

Mapigano hayo yamewalazimu mamia ya maelfu ya raia wa Syria,wengi wao wa kikurdi kutorokea katika taifa jirani la Uturuki,ambalo kufikia sasa limekana kutekeleza mashambulizi ya ardhini dhidi ya wapiganaji wa IS.

Vikosi vya kikurdi vinavyosaidiwa na wanajeshi wa muungano wa Marekani ,wamesema kuwa wanahitaji silaha zaidi na risasi ili kuwasukuma nyuma wanamgambo hao wanaokaribia mji huo.