Malala ashinda tuzo ya amani ya Nobel

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Malala ni mshindi mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kushinda tuzo hiyo

Mwanaharakati mwenye umri mdogo kutoka nchini Pakistan, Malala Yousafzai pamoja na mwanaharakati mwingine wa maswala ya watoto nchini Idnia Kailash Satyrathi, wameshinda tuzo ya amani ya Nobel.

Malala mwenye umri wa miaka 16, ni mshindi mdogo zaidi kuwahi kushinda tuzo hiyo katika historia yake.

Malala amekuwa akiendeleza harakati zake za kutaka watoto wa kike kuweza kupata elimu.

Alipigwa risasi kichwani na kundi la Taleban nchini Pakistan mwaka 2012 kwa kutetea wasichana kupata elimu.