Wanawake kutoana jasho Namibia

Haki miliki ya picha Getty
Image caption soka ya akina dada

Timu za kitaifa za soka ya akina dada kutoka mataifa ya Nigeria, Ghana na Cameroon zitamenyana katika kombe la mabingwa Afrika upande la wanawake ambalo limepangwa kuanza hapo Jumamosi nchini Namibia.

Dimba hilo litafanyika hapo tarehe 11 hadi 25 oktoba mwaka huu na mechi zote zitachezewa katika viwanja viwili; kile cha The Independence stadium na Sam Nujoma Stadium mjini Windhoek.

Timu zitakazofuzu katika mchuano huo ndizo zitakazoshiriki katika kombe la dunia la wanawake litakalofanyika nchini Canada hapo tarehe 5 mwezi Juni hadi tarehe 5 Julai mwaka ujao.

Timu tatu bora katika mashindano hayo yatakayochukua majuma mawili, ndiyo itakayowakilisha bara la Afrika huko Canada.

Haki miliki ya picha NFF
Image caption wachezaji wa nigeria

Timu kubwa kama vile Super Falcons ya Nigeria, Black Queens ya Ghana na Indomitable Lionesses ya Cameroon zinatarajiwa kuzitoa jasho timu za mataifa mengine matano yanayoshiriki katika kinyang'anyiro hicho ili kujipatia nafasi ya kufika fainali.

Hata hivyo, hali huenda ikawa ngumu kwani timu kama vile Brave Gladiators, Banyana Banyana, Chipolopolo Queens, Les El├ęphantes na Les Fennecs Dames huenda zikajinyakulia nafasi hiyo ya kushiriki kombe la dunia kutokana na makali yake. . Kundi A: Namibia, Nigeria, Ivory Coast and Zambia

Timu ya Super Falcons kutoka Nigeria inatazamiwa kuongeza makali yake ili kufanya vyema mjini Windhoek. Hii ni baada ya kutofanya vyema katika dimba lililopita, walipomaliza katika nafasi ya nne katika orodha ya timu bora.

Matokeo hayo ndiyo mabaya zaidi kuwahi kurekodiwa katika historia ya mashindano hayo.

Ikiwa ndiyo timu iliyo na mafanikio zaidi kwani imeshinda kombe hilo mara sita na kukosa mara mbili katika mwaka wa 2008 na 2012 waliposhindwa na wenyeji Equatorial Guinea katika fainali zote mbili.

Super Falcons inatazamiwa kufuzu kwa urahisi katika mashindano ya makundi kwani ipo pamoja na timu dhaifu kama vile Zaimbia na Namibia.