Mashua yazama na kuwaua watu 9 Guinea

Haki miliki ya picha AFP
Image caption boti yazama

Mashua moja imezama kwenye mto moja nchini Guinea ambapo watu tisa wameaga dunia huku wengine kadha wakiwa hawajulikani waliko.

Ripoti zinasema kuwa ajali hiyo ilitokea ijumaa jioni katika eneo la kusini mashariki mwa nchi hiyo karibu na mpaka na Sierra Leone.

Maafisa wanasema kuwa watu 18 kati ya watu 69 waliokuwa kwenye mashua hiyo walikuwa wameokolewa kabla ya usiku kuingia.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Theodore nguema

Wakati huohuo..makamu wa rais nchini Equatorial Guinea amelazimika kuachia mali yenye thamani ya dola milioni 30 iliyo nchini Marekani ambayo utawala wa nchi hiyo unasema kuwa ilinunuliwa kwa pesa za wizi.

Theodoro Nguema Obiang atalazimika kuuza mali yake likiwemo jumba la kifahari kwenye mji wa Malibu , gari aina ya Ferrari na sanamu sita za mwanamuziki Michael Jackson.

Hata hivyo Marekani haijafanikiwa kutwaa mali ya bwana Obiang nchini Equatorial Guinea ikiwemo ndege ya kibinafsi.

Idara ya mahakama nchini Marekani inasema kuwa hatua hiyo inaonyesha kwamba hakuna maficho salama ya mali ya wizi nchini Marekani.