Wakutana kujadili ujenzi wa Gaza

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Viongozi wakutana Misri

Wawakilishi wa zaidi ya nchi 50 wanakutana mjini Cairo hii leo katika mkutano wa kulijenga upya eneo la Gaza baada ya vita vya hivi majuzi kati ya Hamas na Isreali.

Utawala wa Palestina unataka usaidizi wa dola biliioni nne kufadhii ujenzi wa miaka mitatu.

Gaza ilikumbwa na uharibifu mkubwa wa miundo msingi yake wakati wa mzozo huo.

Sehemu zingine zilikuwa zikionekana kama zile zilizokumbwa na tetemeko la ardhi baada ya mashambulizi ya Israeli yaliyokuwa na lengo la kusitisha mashambulizi ya roketi kutoka kwa wanamgambo wa Hamas

Mwandishi wa BBC mjini Cairo anasema kuwa ahadi kadha zinatarajiwa lakini ujenzi utafanyika kulingana na vile Israeli itakavyoruhusu kuingizwa kwa bidhaa za ujenzi ambazo awali zimetumiwa na Hamas kujenga barabara za chini kwa chini.