Ban Ki-Moon afanya ziara ya ghafla Libya

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ban Ki Moon

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki Moon ametoa wito wa kudumishwa kwa amani nchini Libya baada ya kufanya ziara ya ghafla mjini Tripoli kama hatua ya Umoja wa Mataifa kuleta maridhiano nchini humo.

Katika ziara yake ya kwanza mnamo mwaka 2011 ,wakati marehemu Kanali Muamar Gaddafi alipopinduliwa ,aliwaambia wabunge katika hoteli moja mjini humo kwamba hakuna hatua nyengine mbadala ya maridhiano.

Waziri wa maswala ya kigeni nchini Italy Federica Mogherini aliandamana na mkuu huyo.

Umoja wa mataifa ulianzisha makubaliano ya kuleta amani kati ya wabunge pinzani baada ya miezi kadhaa ya machafuko.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wapiganaji wa makundi pinzani wakabiliana Libya

Ukosefu wa amani umelifanya taifa hilo lenye utajiri wa mafuta kukosa udhabiti huku bunge jipya lilochaguliwa mwezi July likilazimika kufanya vikao vyake nje nao wapiganaji kutoka makundi pinzani yakipigania udhibiti wa mji huo.

Bwana Ban na Bi Mogherini waliwasili mjini Tripoli kwa ndege kutoka taifa jirani la Tunisia ,ambapo ubalozi wa umoja wa mataifa nchini Libya umekita kambi tangu uondolewe nchini humo wakati wa msimu wa joto.

''Libya inahitaji bunge na serikali yenye uwezo'',bwana Ban aliwaambia.Mapigano ni sharti yasitishwe...tusitishe umwagikaji wa damu.

Bi Mogherini ambaye anatarjiwa kuwa mkuu wa sera za kigeni katika muungano wa Ulaya mwezi ujao aliliunga mkono bunge la Libya.