Hamilton mshindi wa Russia Grand Prix.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Lewis Hamilton na furaha ya ushindi

Dereva raia wa Uingereza wa mashindano ya mbio za magari langa langa Lewis Hamilton ameshinda mbio za magari hayo huko Urusi yanayojulikana Russia Grand Prix. Hamilton ameiambia BBC kwamba anafuraha sana na 'mwisho wa wiki wa ajabu' baada ya kushinda mbio hizo. Ushindi huo Hamiltoni ni wa tisa na umesaida wakandarasi wa magari ya Mercedes katika ushindi wake wa mwanzo pamoja na ushindi wa dunia wa mwaka 2008 kuitukuza 'kazi ya kushangaza' iliyofanywa na timu. Mchezaji mwenzake wa timu ya Mercedes Nico Rosberg sasa anamfuatia Hamilton kwa point 17 huku michezo mitatu ikisalia point 100.