Waasi wa M23 wakana kutenda uovu

Haki miliki ya picha
Image caption Jean Marie Runiga kiongozi wa kisiasa wa M23

Kundi la wasi la M23 ambalo limekuwa mashariki mwa DRC limekanusha madai ya kufanya uovu kama vile mauaji ya kiholelela pamoja na ubakaji katika maeneo ambayo kundi hilo lilikuwa likidhidhiti.

Wapiganaji hao walishindwa na majeshi ya serikali ya DRC yakisaidiwa na kikosi cha kulinda amani cha MONUSCO

Kwa upande wake linakilaumu kikosi cha MONUSCO kwa kushindwa kutekeleza kazi zake.Kwa sasa wapiganaji na maofisa wa kundi hilo wako Uganda ambako walikimbilia.

Kundi la M23 limetoa taarifa kukanusha rasmi ripoti ya shirika la kutetea haki za binadamu la Umoja wa Mataifa nchini DRC ambayo ilisema kuwa uchunguzi uliofanywa eneo la Kivu Kaskazini waonyesha kama kundi la M23 lilifanya maovu kama vile ubakaji na vigogo wa Umoja huo kutaka hatua muafaka kuchukuliwa dhidi ya waliohusika na visa hivyo.

Eneo hilo lilikuwa chini ya udhibiti wa kundi la M23 kati ya April 2012 hadi Oktoba 2013 baada ya kutimuliwa.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa inasema kuwa M23 iliua watu 160 na kubaka wanawake 161 kati ya kipindi hicho.

Ripoti yenyewe imechapishwa na ofisi ya pamoja inayohusika na haki za binadamu nchini DRC na wala sio MONUSCO, lakini kwa nini kundi la M23 kila kosa dhidi yao wanailaumu MONUSCO.

Katika taarifa iliotolewa makao makuu ya tume haki za binadamu ya ya Umoja wa Mataifa imenukuu kinarawake-Zeid Raad Al Hussein akipongeza utawala wa Kinshasa kwa kuwafungulia mashtaka baadhi ya watu wanaodaiwa kuhusika katika kesi kama hizo wa kundi la M23 na kuwahimiza kuendelea na juhudi zao kuhakikisha kuwa wale wanaoshutumiwa kufanya makosa makubwa wanatendea haki.

Kundi la M23 lilifurushwa na majeshi ya serikali yakisaidiwa na yale ya MONUSCO kutoka maeneo lilikokuwa likidhibiti kama vile Goma na pia maeneo ya mpaka na Uganda tangu Aprili 2012.Wapiganaji wake wengi pamoja na viongozi wake walikimbilia Uganda ambako wanaishi hadi sasa.