Mapambano dhidi ya Ebola ni hafifu

Haki miliki ya picha
Image caption Mgonjwa wa Ebola

Viongozi wakuu wa Umoja wa mataifa wanajishughulisha na ugonjwa wa Ebola wameutaka ulimwengu kuwa na subra,na kueleza kuwa adui mkubwa katika mapambano ya kuutokomeza ugonjwa wa Ebola ni muda.

Akihutubia mkutano huo kutoka Africa Magharibi kutoka Africa Magharibi, Antony Banbury ameeleza kuwa katika harakati za kupambana na Ebola ,virusi vya ugonjwa huo vinaelekea kuwa na nguvu zaidi.

Ingawa ametahadharisha na kutoa mtazamo kuwa mpaka kufikia December mwaka huu kutakua na idadi kubwa ya vifo na wagonjwa wapya,lakini pia anaamini mipango mipya pia ya kupambana na ugonjwa huo pengine ni hafifu na hivyo kuongeza maafa zaidi.

Kutokana na kauli hiyo Antony ametaka misaada zaidi ya kifedha ielekezwe Afrika Magharibi ili kujenga vituo zaidi vya afya huko katika nchi zilizo athiriwa zaidi na ugonjwa huo za Sierra Leone, Guinea na Liberia pamoja na kuongeza idadi ya wafanyakazi wa afya .

Naye Rais wa Marekani Barck Obama ametoa wito wa kuongeza umakini katika ugonjwa huo katika mkutano wa ulinzi na usalama ,kwamba juhudi za ulimwengu katika kupambana na ugonjwa huo hazitoshi.