Hong Kong si shwari tena

Haki miliki ya picha BBC CHINESE
Image caption Polisi wa Hong Kong

Waandamanaji wanaodai demokrasia nchini Hong Kong wame zushga rabsha baina yao na polisi wakati hali ya amani bado ni tete ikiwa ni zaidi ya wiki tatu sasa waandamanaji hao kuwa katika mitaa ya nchi yao kudia uhuru wa kujichagulia kiongozi wamtakaye.

Polisi waliingia mtaani kutaka kuwaondosha waandamanaji hao amabao wamekusanyika mbele ya ofisi kuu za serikali mjini humo.

Polisi walipamna na waandamanaji hao kwa kutumia hewa za makaratasi,na inaarifiwa kuwa wataandamanaji kadhaa walijeruhiwa katika mapambano hayo na wengi wao wamekamatwa.

Waandamanaji hao wameufunika mji huo wa Hong Kong ,wakidai kuwa uchaguzi wa kiongozi ajaye lazima uwe wa kidemokrasia.