Mashambulizi ya Kobane yamkera Obama

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mji wa Kobane katika mashambulizi

Rais Barack Obama amewaambia makamanda wa ngazi ya juu wa jeshini kwamba ameguswa na kile kinachoendelea ambacho wanamgambo wa dola ya kiislam wa IS wanafanya kinyume na mji wa Kobane huko Syria.

Rais Obama pia amegusia wanamgambo wa kujitoa muhanga walioko magharibi mwa jimbo la Anbar,aliuambia mkutano unaofanyika karibu na mji wa Washngton kwamba kampeni zinazoendelea dhidi ya wanamgambo wa dola ya kiislam kwamba ni za muda mrefu ,ukijumuisha mipango, changamoto za awali na maendeleo yake.

Mkutano huo unahudhuriwa ma maafisa wa ngazi za juu kutoka nchi zaidi ya ishirini, ambapo mwanzoni mwa mkutano huo wizara ya ulinzi ya Marekani imeelezea mipango ya mashambulizi ya anga dhidi ya wanamgambo wa dola ya kiislam karibu na mji wa Kobane kwamba ni ya mafanikio makubwa.