Ni kinyang'anyiro kikali Msumbiji

Haki miliki ya picha
Image caption mitaa ya nchi ya Msumbiji

Wapiga kura wanaelekea kwenye vituo vya kupigia kura nchini Musumbiji leo kumchagua rais mpya na wabunge kwenye uchaguzi wenye upinzani mkali tangu taifa hilo lipate uhuru mwaka 1975.

Takriban watu 11 wamejiandikisha kupiga kura nchini humo wakiwemo wengine 90,00 wanaoishi mataifa ya kigeni.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Mambango yamekuwa yakishuhudiwa kila sehemu ya mji mkuu wa Msumbiji

Zaidi ya watu milioni 10 wamejiandikisha kupiga kura katika uchaguzi wa leo, ambao unaonekana kuwa wa kwanza kidemokrasia tangu nchi hiyo ilipojipatia uhuru wake kutoka kwa Wareno mwaka 1975.

Chama tawala, cha Frelimo, ambacho kimekuwa mamlakani tangu mwaka 1975, kinakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa chama cha upinzani cha Renamo.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Rais Arrnando Guebuza (kushoto) na muasi wa zamani wa Renamo Afonso Dhlakama walifikia mkataba wa amani Septemba

Kiongozi wa Renamo,Afonso Dhlakama, alitoka mafichoni mwezi jana na kuingia katika kinyang'anyiro cha uchaguzi mkuu katika dakika za mwisho baada ya kufikia makubaliano ya amani na serikali.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Mamilioni ya watu wamesajiliwa kupiga kura

Mgombea wa chama tawala ni Filipe Nyusi, ambaye ni waziri wa zamani wa ulinzi.

Msumbijini moja ya nchi zinazokuwa kwa kasi barani Afrika na mshindi wa uchaguzi atahakikisha rasilimali za nchi ikiwemo gesi zinatumiwa vyema.