Utoaji mimba wazua gumzo Marekani

Image caption Sheria hiyo tatanishi iliidhinishwa na gavana Rick Perry mwaka 2013

Mahakama ya juu zaidi nchini Marekani, imetupilia mbali vifungu kadhaa vya sheria tatanishi inayowekea vikwazo wanaotaka kutoa mimba.

Mahakama hiyo imefutilia mbali uamuzi wa mahakama ndogo inayozitaka hospitali za serikali kutumia kiwango kikubwa cha pesa kupandisha daraja hospitali zao na kuongeza huduma za kutoa mimba.

Mahakama hiyo ndogo ingali inatathmini uhalali wa sheria hiyo iliyotiwa saini na gavana Rick Perry mnamo mwaka 2013.

Uamuzi huo una maana kuwa kliniki nyingi zilizofungwa ambako wanaweza walikuwa wakitolea mimba zinaweza kufunguliwa upya, hatua ambayo imepongezwa na wanaharakati wanaopigia debe swala la kutoa mimba.

"tuna afueni maana mahakama iliingilia swala hili na kufutilia mbali sheria hiyo, na tunatumai kuwa sheria hii hatari inaweza kufutiliwa mbali kabisa,'' alisema Cecile Richards, mkuu wa shirikisho la uzazi wa mpango nchini Marekani.

Image caption Sheria ya utoaji mimba katika jimbo la Texas imezua hisia kali

Ikiwa sheria hio ingepitishwa, kliniki nane za kutoa mimba zingefungwa katika jimbo hilo la pili katika wingi wa idadi ya watu nchini Marekani.

Kati ya majaji wanane wa mahakama ya juu zaidi, sita waliunga mkono haki za wanaotaka kuhalalisha utoaji mimba.

Wanasiasa wenye msimamo mkali wa chama cha Conservative wanasema kuwa sheria hiyo inalenga kuwalinda wanawake lakini wakosoaji wake wanasema kuwa sheria yenyewe ni njama ya kuharamisha utoaji mimba, ambayo ni haki inayopewa na katiba ya nchi tangu mwaka 1973.

Mnamo mwezi Agosti, jaji mmoja kwa jina Lee Yeakel, alisema kuwa sheria hiyo hailengi kuhakikisha kuwa wanawake wanakuwa salama bali kudhibiti huduma za utoaji mimba katika jimbo hilo.

Nyingi ya kliniki za kutoa mimba zimefungwa kutokana na sheria hiyo ambayo inasema madaktari ambao kazi yao ni kutoa mimba wasiruhusiwe kuendesha shughuli zao katika hiospitali nyingi.