Nigeria yaibwaga Zambia yaingia nusu fainali

Haki miliki ya picha AP
Image caption Kikosi cha Nigeria -wanawake

Nigeria imeibamiza bila huruma Zambia kwa mabao sita kwa nunge katika mchezo wa mpira wa miguu kwa wanawake katika michuano ya klabu bingwa barani Africa na kutinga nusu fainali huko nchini Namibia.

Kwa mara ya sita mfululizo Nigeria ilitia maguu katika nusu fainali hiyo kama kumsukuma mlevi kiulainii mapema wiki hii wakiwa kundi A , wakiwa na wachezaji mahiri kama Desire Oparanozie aliyefunga mabao ya kutosha wakiwemo Ngozi Okobi, Osinachi Ohale, Asisat Oshoala na Perpetua Nkwoch ambao wote kila mmoja alizifumania nyavu kwa wakati wake.

Katika kipigo hicho cha hata kufurukuta wakina dada hao wa timu ya Chipolopolo, mchezaji wake wa upande wa kulia Grace Zulu alitolewa dimbani dakika sita kabla ya mapumziko .

Nigeria ilifungulia karamu ya mabao dakika mbili baada ya mchezo kuanza wakati Okobi alipoonana vizuri na Asisat Oshoala karibu kabisa na eneo la hatari .

Dakika tatu baadaye Ohale aliparaza mpira kwa kichwa katika mpira wa adhabu ndogo wakati ambapo Oparanozie alipozifumania nyavu baada ya penati kwa kuunawa mpira , Nigeria walikua wameumiliki mpira vilivyo.

Ni Tia aliyekuwa wapili kuzifumania nyavu wakati wa dakika za majeruhi kabla ya kuingia mapumziko alipoutia kimiani mpira huo kwa kuubabatiza kutokana na mpira wa adhabu ndogo .

Juhudi za timu ya Zambia za kutaka kufurukuta katika mchezo huo hazikuzaa matunda baada ya mchezaji wake Zulu kuwa wa pili kutolewa nje ya uwanja baada ya kulamba kadi ya njano kwa kumchezea rafu mchezaji wa Nigeria Oparanozie.

Baada ya kipindi cha mapumziko kikosi hicho cha Super Falcons kutoka Nigeria kilizitumia hesabu walizofundishwa shuleni kuonana vyema uwanjani nazo zikalipa pale ambapo shoala alichomoka na kona ya hatari na kuandika bao la nne bila majibu.

Super Falcon walifanikiwa kuwavuruga vilivyo timu ya wanawake ya Chipolopolo kwa bao la sita lililokwamishwa wavuni na mchezaji wake Oparanozie baada ya kuingia kwa mchezaji Perpetua Nkwocha aliyekamilisha karamu ya magoli.

Kwa matokeo hayo Nigeria ikajizolea pointi sita zilizotakata ambapo sasa Nigeria itaikaribisha timu ya Namibia mwishoni mwa wiki hii katika mechi ya hitima.

Wakati huo huo si vibaya ukijua msimamo wa timu ya Namibia kwamba ilishanyukwa mabao 3-1 kwa Ivory Coast mapema wiki hii ,ambapo sasa Namibia endapo itaokota dhahabu mtaani kwa kuifunga Nigeria na kama wa Ivory Coast watashindwa kuwafunga Nigeria basi watabaki katika nusu fainali mechi zitakazopigwa mwishoni mwa wiki.

Hata hivyo,watatetea nafasi yao kwa mabao mawili waliyofunga dakika za lala salama za mchezo baina yao na Namibia na kuwapa nafasi mataifa hayo mawili kwa pointi tatu.

Ni mchezaji Estelle Nah,wa Nigeria aliyekua nyota wa mchezo huo siku chache tu baada ya kuachiliwa na timu yake ya Russian club, WFC Zvezda,aliyeupamba vilivyo mchezo huo na kufungua karamu ya mabao katika dakika 13 tu baada ya mpira wa adhabu ndogo kutoka kwa mchezaji Josephine Leyo kurudi dimbani