Maelfu ya magari ya Toyota yana hitilafu

Haki miliki ya picha bbc
Image caption Sio mara ya kwanza kwa Toyota kuagiza magari yake kurejereshwa kwa ajili ya hitilafu

Kampuni kubwa zaidi ya kuunda magari, Toyota, imeagiza kurejeshwa kwa magari milioni moja nukta saba kote duniani kutokana na hitilafu ya breki za magari hayo.

Kampuni hiyo imesema hitilafu tatu zimetambulika kwenye breki katika miundo mbali mbali za magari ya Toyota ikiwemo muundo wa Lexus.

Magari yaliyo ndani na nje ya Japan yote yameathiriwa na hitilafu hizo.

Hata hivyo kampuni yenyewe imesema haina habari yoyote kuhusu ajali za magari au watu kujeruhiwa kutokana na hitilafu hizo.

Wadadisi wanasema hili ni jambo la kuabisha sana kwa Toyota ambayo imelazimika kuagiza magari yake kurejeshwa kiwandani zaidi ya mara moja kutokana na hitilafu mbali mbali.