Ebola:Ahadi za mataifa hazijatimizwa

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Shirika la MSF ndilo linafanya kazi kubwa kuwaaidia wagonjwa wa Ebola Afrika Magharibi

Shirika la madaktari wasio na mipaka la Medecins Sans Frontieres ambalo ndilo shirika kuu linalopambana na ugonjwa wa Ebola Magharibi ya Afrika , linasema kuwa ahadi za kimataifa za kutoa msaada na kupeleeka wahudumu kwenda eneo hilo havijakuwa na mafanikio yoyote dhidi ya ugonjwa wa ebola.

Mkuu wa shirika hilo Christopher Stokes anasema kuwa ugonjwa wa ebola unaelekea kukosa kudhibitiwa.

Hata baada ya kuwepo ahadi za kimataifa za kusaidia kupambana ugonjwa wa ebola ambazo zinawasili kwa mwendo wa chini , shirika la madaktari wasio na mipaka ndilo bado linaongoza huduma katika vituo vya afyua vinavyotoa matibabu ya ugonjwa huo eneo la afrika magharibi.

Haki miliki ya picha Other
Image caption Maelfu ya watu wamepoteza jamaa wao waliougua Ebola nchini Liberia, Guinea na Sierra Leone

MSF linasimamia zahanati zenye karibu vitanda 700 kati ya vitanda 1000 ambayo vina wagonjwa wanaogua ebola.

Hata hivyo wnegi wanasema kuwa idadi inayohitajika ni mara tatu ya hiyo na ugonjwa huo umeshindwa kudhibitiwa.

Kumekuwa na ahadi za kimataifa kutoka kwa jamii ya kimataifa kwa mfano jeshi la uingereza linajenga hospitali nchini Siera Leone.

Lakini hata hivyo msemaji wa MSF Christopher Stokes anasema kuwa hatua hizo zote huenda zikose kuwa za manufaa makubwa katika kipindi cha kati ya mwezi mmoja na wiki sita.