USA:Hatuamini mkataba na Boko Haram

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Obama

Marekani inasema kuwa haina thibitisho lolote kuhusu mkataba wa kusitisha mapigano uliotangazwa kati ya jeshi la Nigeria na kundi la wanamgambo wa Boko Haram.

Msemaji wa rais nchini Nigeria amesema kuwa makubaliano hayo yalihusu kuachiliwa kwa zaidi ya wasichana 200 wa shule waliotekwa na Boko Haram miezi sita iliyopita.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Boko Haram

Lakini hata hivyo Boko Haram hawajasema lolote lakini mwandishi wa habari raia wa Nigeria anayeishi uhamishoni na anayehusishwa na Boko Haram anasema kuwa kundi hilo limekasirishwa kutokana na kile alichokitaja kuwa njama za kisiasa.

Makubaliano hayo yaliafikiwa baada ya wiki kadha za mazungumzo yalioongozwa na Chad na mikutano zaidi inahitajika ili kuafikia jinsi wasichana hao watakavyoachiliwa.