UN yatetea juhudi za kuangamiza Ebola

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption David Nabarro katikati

Mratibu wa shughuli za Umoja wa mataifa kuhusu ugonjwa wa ebola Davis Nabarro ametetea juhudi za kimataifa za kupambana na ugonjwa huo magharibi mwa afrika.

Bwana Nabbaro alikuwa akijibu shutma kutoka kwa shirika la madaktari wasio na mipaka MSF lililosema kuwa ahadi za misaada hazijakuwa na mafaniko yoyote katika vita dhidi ya ugonjwa wa ebola.

Ameiambia BBC kuwa mipango iko njiani ya kutoa vitanda 4000 kwa wagonjwa wa ebola ifikiapo mwezi ujao.

Matamshi yake yanajiri baada ya ripoti ya ndani ya shirika la afya duniani inayosema kuwa WHO imeshindwa kuzuia kusambaa kwa ugonjwa wa ebola.