Ebola:Meli ya Marekani yazuiwa Mexico

Haki miliki ya picha REUTERS
Image caption Meli

Meli moja ya Marekani imenyinwa ruhusu ya kutia nanga katika kisiwa cha Mexico cha Cozumel kutokana na hofu kuwa mmoja wa abiria wake huenda ana virusi vya ugonjwa wa ebola.

Meli hiyo kwa jina Carnival Magic iliondoka katika jimbo la Texas ikiwa na mhudumu mmoja wa afya ambaye alikuwa amehudumia sampuli za mgonjwa wa ebola marehemu Thomas Duncan aliyeaga dunia kutokana na ugonjwa huo.

Afisa mmoja katika bandari ya Mexico alisema kuwa hatua hiyo ilichukuliwa ili kuzuia kusambaa kwa ugonjwa we ebola.

Mhudumu huyo wa afya ambaye amejitenga pamoja na mumewe wakiwa kwenye meli hiyo yuko chini ya uangalizi kwa ameonyesha dalili za ugonjwa huo.