Rais wa S.Leone abuni kamati ya Ebola

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ernest Koroma

Rais wa Sierra Leone ,Ernest Bai Koroma amechagua kamati mpya ya kukabiliana na ugonjwa wa ebola nchini humo.

Kamati hiyo itaongozwa na waziri wa ulinzi major Alfredo Palo Conteh na ataripoti moja kwa moja kwa rais.

Katika taarifa yake ,bwana Koroma amesema kuwa mabadiliko hayo ni muhimu kutokana na kiwango cha mlipuko wa ugonjwa huo.

Zaidi ya watu 1200 wamefariki kutokana na Ugonjwa huku viwango vya maambukizi vikiongezeka.

Umoja wa mataifa umeanza kusambaza chakula katika mji mkuu wa Freetown,kwa sababu raia wengi wameamua kusalia majumbani ili kuepuka kuambukizwa.

Haki miliki ya picha Unknown
Image caption Obama

Wakati huohuo Rais wa marekani barack obama ameonya kuwa hofu hasitahili kutawala kutokana na kuwepo kwa mlipuko wa ugonjwa wa ebola akisema kuwa marekani haistahili kuweka kwazo vya usafiri kwa nchi za afrika magahribi zilizoathirika zadi na ugonjwa huo

Rais Obama amesema kuwa hatua hiyo itachangia hali iliyopo kuwa mbaya zaidi.

Taarifa hiyo inatolewa wakati vyombo vya habari nchini marekani vinaripoti kuwa bwana Obama aliezea ghadahbu yake kisiri kuhusu jinsi suala ya ebola lilivyoshughulikiwa nchini marekani