Renamo yakubali matokeo ya uchaguzi

Alfonso Dhlakama

Chama kikuu cha upinzani cha Msumbiji, Renamo, ambacho zamani kilikuwa chama cha wapiganaji, kimesema kuwa kitakubali matokeo ya uchaguzi uliofanywa juma hili ingawa kabla kilisema uchaguzi ulikuwa na kasoro.

Kiongozi wa Renamo, Afonso Dhlakama, alisema chama chake kinakusanya yale yaliyoelezwa kuwa ukosefu uliotokea, kama wapigaji kura kutishwa na masanduku ya kura kujazwa kura za uongo.

Matokeo ya awali yanaonesha chama tawala cha Frelimo kinaongoza.

Wasimamizi wa uchaguzi wa kimataifa walisema kulikuwa na visa vya udanganyifu, lakini haikuelekea kuwa vitaathiri matokeo ya mwisho ya uchaguzi.

Bwana Dhlakama ananukuliwa akisema kuwa Renamo haitarudi kwenye vita - " hakuna haja ya kufanya hivyo" alisema