Mazrui hatimaye azikwa

Image caption Ali Mazrui

Msomi maarufu marehemu Profesa Ali Mazrui hatimaye amezikwa.

Mazrui alizikwa nyumbani kwao katika eneo la Old Town mjini Mombasa nchini Kenya.

Mwili wake uliwasili mapema jumapili kutoka nchini Marekani ambako amekuwa akiishi.

Msomi huyo alikuwa na tajriba kuu katika taaluma yake.

Mbali na kuwa mwalimu alisomea katika vyuo vikuu ikiwemo Oxford ambapo alijapatia shahada ya philosophia mwaka 1966.

Baadaye Mazrui alijiunga na Chuo kikuu cha Makerere kama mkuu wa kitengo cha sayansi ya siasa.

Vilevile ameweza kuandika vitabu chungu nzima ambavyo vitaendelea kuwa kumbukumbuku yake.