Mapigano yaanza tena Nigeria

Haki miliki ya picha afp
Image caption Boko Haram

Taarifa kutoka Kaskazini Mashariki mwa Nigeria zinasema zaidi ya watu ishirini wameuawa katika mapigano kati ya wanajeshi na wanamgambo wa kundi la Boko Haram, licha ya makubaliano ya kusitisha vita kufanyika ijumaa iliyopita.

Vurugu zilifanyika siku ya katika mji wa Damboa. Makubaliano ya kusitisha vita kati ya wanamgambo wa Boko Haram na serikali ya Nigeria yanatarajiwa kuwaokoa wasichana zaidi ya mia mbili waliotekwa na kikundi hicho mwezi Aprili mwaka huu.

Mwandishi wa BBC nchini Nigeria anasema mapigano hayo yameleta hali ya wasiwasi kuhusiana na uwezekano kusitisha mapigano hayo.