Australia yabadili kauli kuhusu Burka

Image caption Wnawake waisilamu wanasema serikali imenua kuwabagua

Serikali ya Australia imebatilisha uamuzi wake ambao unawazuia wanawake wanaovalia Burka au kujifinika nyuso zao na kuwacha sehemu ya mcho peke yake kuingia bungeni mjini Canberra.

Mapema mwezi huu, bunge lilisema kuwa yeyote anayeingia katika jengo hilo uso wake ukiwa umefunikwa atalazimika kuketi katika sehemu iliyotengewa wananchi.

Hatua hiyo ilionekana na wengi kama ilyowalenga wanawake waisilamu na kuzua hoja kuhusu ubaguzi.

Maafisa wanasema wageni sasa watalazimika kuwaonyesha maafisa wa usalama nyuso zao kabla ya kuingia bungeni.

Mpango huo wa bunge ungewaathiri wanawake waisilamu wanaovalia Niqab ambapo hakuna sehemu ya uso wao inayoonekana.

Rais wa baraza la Senate, Stephen Parry, alisema uamuzi wa kwanza ulitolewa kwa sababu ya fununu kuwa kikundi cha watu waliokuwa wamefunika nyuso zao walikuwa wanapanga kuvamia kipindi cha maswali na majibu tarehe 2 Oktoba kinachoendeshwa na waziri mkuu katika bunge hilo.

Alisema kuwa hatua zilizochukuliwa zilinuia kuwa za mda tu na kuzuia vurugu bungeni.

Waziri mkuu Tony Abbot, alitaja Burka kuwa vazi linalowatisha watu wengi, na kwamba anatamani ikiwa watu wasingekuwa wanavalia vazi hilo.

Agizo hilo liliwekwa baada ya kuwepo wasiwasi kuhusu uwezo wa shambulizi