Ebola na utaratibu mpya wa Mazishi

Haki miliki ya picha epa
Image caption Madaktari wa Ebola

Ugonjwa wa Ebola unahitaji hatua za haraka na umakini katika kuhifadhi miili ya watu waliopoteza maisha kutokana na ugonjwa huo.

Hii ina maana kuwa hatua hiyo inaondokana na taratibu za kawaida zilizozoeleka za mazishi katika nchi zilizoathirika, ikiwemo matumizi ya mifuko mikubwa ya plastiki ambayo ni mbadala wa majeneza.

Mabadiliko haya yanawaathiri wafanyabiashara wanaojipatia kipato kwa kutengeneza majeneza na wanaotoa huduma za mazishi Taarifa yake Mwandishi wa BBC mjini Monrovia nchini Liberia amebaini kuwa biashara hiyo imedorora.

Wafanya biashara wa majeneza wanasema kutokana na kuwepo kwa ugonjwa wa Ebola wateja hawapatikani kwa wingi sababu ikielezwa kuwa watu waliopoteza maisha huhusishwa na maradhi ya ebola.

Serikali ya Liberia imesema kuwa watu waliokufa hawatazikwa wakiwa ndani ya majeneza isipokuwa kwenye mifuko mikubwa ya Plastiki.