Harakati za Ulaya dhidi ya Ebola

Haki miliki ya picha Thinkstock
Image caption Virusi vya ugonjwa wa Ebola

Mawaziri wa mambo ya nje wa muungano wa ulaya wanakutana hii leo kujadili mikakati ya kudhibiti maambukizi ya Ebola .

Zaidi ya watu 4,500 wamekufa kutokana na mlipuko wa ugonjwa huo wengi wao raia wa Afrika Magharibi .

Huku idadi ya visa vya Ebola ikiendelea kuongezeka, hii imekuwa ni changamoto ya moja kwa moja inayokabili mawaziri wa mambo ya nje kutoka muungano wa ulaya .

Wanakutana mjini Luxembourg wakiwa na fikra ya dhahurura kwamba juhudi zinahitajika katika kudhibiti kuenea kwa virusi vya ugonjwa huo hatari.

Uingereza imeahidi kutoa zaidi ya pauni milioni 100 katika juhudi hizo , mataifa ya ulaya kwa ujumla yameahidi kutoa takriban pauni milioni 400 .

Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron anataka juhudi hizi ziongezwe mara dufu.

Pesa hizo zitasaidia mataifa ya Liberia, Sierra Leone na Guinea kuimarisha mifumo duni ya afya nchini humo na kukabiliana na hasara za kiuchumi zilizotokana na Ugonjwa huo .

Hata hivyo imebainika kuwa bado kikosi cha askari, vifaa vya maabara na ujenzi wa hospitali ni huduma zinazohitajika huko zaidi .