Taliban waanzisha mapigano Afghanistan

Haki miliki ya picha none
Image caption Wapiganaji wa Talban

Serikali ya Afghanistan imesema mamia ya wapiganaji wa Taliban wamevamia na kuanzisha mapigano kwenye maeneo mawili ya Afghanistan ya kati na mashariki mwa nchi hiyo.

Katika jimbo la Logar, wanamgambo walivamia baadhi ya maeneo ya malindo makuu.

Mapigano yameendelea zaidi ya saa kumi huku wanajeshi wanne wakiripotiwa kuuawa katika mapambano hayo. Mawasiliano katika eneo yameharibiwa kufuatia na mapigano hayo.

Hata hivyo Gavana wa jimbo la Ghor ameiambia BBC kuwa kati ya wanamgambo mia nne hadi mia tano wamevamia vijiji viwili katika nchi hiyo. Mapigano yanaendelea na idadi ya wahanga wa mapigano hayo haijapatikana rasmi.