Marekani yawadondoshea wakurdi silaha

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wapiganaji wa Islamic State

Ndege za kijeshi za Marekani zimedondosha silaha na vifaa vya matibabu kwa wapiganaji wa kikurdi wanaolinda mji wa Kaskazini mwa Syria wa Kobane kutoka kwa wapiganaji wa Islamic State .

Mashambulizi ya anga ya Marekani yamesaidia kuwasukuma nyuma wapiganaji wa Islamc state wanaotaka kuchukua udhibiti wa mji huo uliopo karibu na Uturuki .

Jana rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, aliidhinisha kupelekwa kwa silaha kwa wakurdi , licha ya kwamba mji wa Kobane uko kwenye mpaka na Uturuki . Alikielekeza chama cha kidemoKrasi cha Uturuki ambacho vugu vugu lake linapigana dhidi ya IS kama kundi la ugaidi.

Hii ni mara ya kwanza kudondosha silaha tangu kampeni kali ya mashambulizo yanayoongozwa na Marekani kuanza mwezi uliopita.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Uturuki imekosoa Marekani kwa kutoa silaha kwa wapiganaji wa Kurdi

Makao Makuu ya Kijeshi ya Marekani, Pentagon, yanasema kuwa silaha, risasi na vifaa vingine vya kijeshi vilidondoshwa kando ya mji huo uliovamiwa.

Hatua hiyo imechukuliwa siku moja tu baada ya Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogon, kuonya Marekani isiwape silaha Wakurdi, ambao iliwataja kuwa "Magaidi".

Ni dhahidi kuwa Uturuki inatofautiana pakubwa na muungano wa NATO, ambao yeye ni mwanachama, juu ya msimamo wa muungano huo juu ya Syria.

Serikali ya Uturuki imekataa kuwaruhusu Wakurdi au silaha kupitishwa hadi Sysia kuwasaidia wapiganaji Wakurdi, ikidai kuwa wapiganaji hao ni sehemu moja ya waasi wanaopigana nchini Uturuki wa chama cha Wakurdi cha PKK , ambao wamepigana muda mrefu nchini Uturuki.

Haki miliki ya picha b
Image caption Wakurdi wamekuwa wakihangaika kutokana na vita vinavyoendelea Syria na Iraq

Marais wa Uturuki na Marekani waliongea kwa simu Jumapili, ambapo inakisiwa kuwa walizungumza juu ya uwezekano wa kudondosha vifaa hivyo vya kijeshi.

Lakini inaonekana kuwa hapakutokea makubaliano.

Uhasama mkubwa ulioko kati ya Serikali ya Uturuki na wapiganani Wakurdi umevuruga mpango wa kupambana na Islamic State nchini Syria.

Marekani inasema kuwa inatambua hali liyomo Uturuki kama mmoja wa wanachama wa NATO lakini ni dhahiri kuwa Uturuki imetambuliwa kama taifa ambalo limepuuza wajibu wake katika muungano huo.