Wastani wa Joto wapanda:Utafiti

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Hali ya hewa

Watalaam wa hali ya hewa wa marekani wamesema wastani wa joto la dunia la mwezi uliopita lilikuwa la kiwango cha juu kabisa tangu kuanza kwa ufuatiliaji huo.

Wafuatiliaji wa masuala ya hali ya hewa wamesema iwapo joto litasalia hivyo kwa kipindi cha mwaka kilichobaki basi mwaka 2014 utakuwa umeweka rekodi ya namna yake.

Huko Bonn katika ufunguzi wa mazungumzo yanayohusu hali ya hewa, Mkuu wa Kitengo cha hali ya hewa Christiana Figueres amewaambia washiriki kuwa kuna umuhimu wa kuunganisha nguvu iwapo wanataka kupambana na uchafuzi wa hali ya hewa unaoweza kusababisha ongezeko la joto duniani.