Watafiti na dawa ya Ebola, A.Magharibi

Image caption Kampeni ya Ebola

Shirika la afya ulimwenguni WHO limesema dawa ya Ebola ambayo imetengenezwa kwa mchanganyiko na damu ya watu waliambukizwa na kisha kupona ugonjwa wa Ebola inatarajiwa kuanza kupatikana wiki chache zijazo huko Afrika Magharibi.

Afisa mwandamizi wa W.H.O. Dr Marie Paule Kieny amesema vifaa vimetolewa Liberia kwaajili ya kupata damu na vifaa vya kufanyia utafiti huo wa dawa ili kupata dawa Serum.

Dr Kieny akizungumza mjini Geneva amesema kuwa kazi ya mapambano dhidi ya Ebola harakati za upatikanaji chanjo ya ugonjwa huo .

Maelfu ya watu wanatarajiwa kutumiwa katika majaribio hayo yanayolenga kupatikana kwa chanjo na dawa ya ugonjwa huo.