Wandishi 2 mahakamani Somalia

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Abdi Malik Yusuf (kulia) na Mohammed Bashir (kushoto)

Wandishi wawili wa habari wamefikishwa mahakamani mjini Mogadishu Somalia wakituhumiwa kwa kuhatarisha usalama wa nchi.

Mmiliki wa kituo kimoja cha redio,Radio Shabelle, (Abdi Malik Yusuf) aliachiliwa kwa dhamana wakati mwandishi mwingine akisalia mikononi mwa polisi.

Kesi hiyo imeahirishwa kwa wiki mbili.

Walikuwa miongoni mwa wandishi wengine wanne waliokamatwa mwezi Agosti baada ya kuripoti kuhusu mpango wa kuwapokonya silaha watu mjini Mogadishu.

Maafisa wakuu wanasema kuwa wandishi wa habari walikuwa wameonywa dhidi ya kuripoti taarifa yoyote kuhusu mpango huo wa kuwataka watu kusalimisha silaha zao.

Vyombo vya habari nchini humo vimetoa wito wa kutaka wandishi hao kuachiliwa.