Maswala ya usalama mitandaoni TZ

Image caption masuala ya mtandao kwa computer mpakato

Nchi ya Tanzania imepata bahati ya kipekee kuwa mwenyeji wa warsha ya Kimataifa ya maswala ya usalama mitandao iliyo shirikisha mataifa mbali mbali kujadili na kuongezeana uwezo wa jinsi wa kukabiliana na changamoto kubwa katika maswala ya uhalifu mitandao.

Kila kunapokucha si ajabu kusikia kumekuwa na matukio ya udukuzi au wizi wa mtandaoni. Huko Tanzania wataalam wa maswala ya usalama wa mtandaoni wanakutana kujadiliana mbinu na maarifa za kukabiliana na uhalifu huo

Mkutano huu wa kimataifa unawakutanisha wataalam kutoka mataifa mbali mbali duniani kwa lengo la kufahamu hatari zinazotokana na matumizi ya mitandao na pia kuhadili mbinu za

Nchi hizi zipatazo kumi ikiwemoUganda,Nigeria,Misri,Pakistan,Yemen,Jordan,Senegal,Soud Arabia,Zanzibar na wenyeji Tanzania wanakutana ili kuunganisha nguvu za pamoja kwenye vita dhidi ya uhalifu wa mtandao ikizingatiwa uhalifu mtandaoni ni uhalifu usio mipaka na kuna mahitaji makubwa ya kushirikiana katika taarifa na utaalam.

Wito Mkubwa ulitolewa na katibu mkuu wa wizara ya sayansi mawasiliano na teknolojia nchini Tanzania profesa Patrick Makungu kuwataka wataalam na washiriki wengine kutochoka na kuongeza jitihada kukabiliana na wimbi la uhalifu mtandaoni linalokua kwa kasi duniani kote ili kuweza kuwa mbele ya wahalifu mitandao kupitia hotuba aliyo isoma kwa niamba ya Waziri wa Wizara hiyo .

Aidha, Mkurugenzi mkuu wa COSTECH, Dr. Hassan Mshinda alisema nifursa nzuri sana kwa watanzania na kuanisha ni mikakati endelevu yakuendelea kukuza uwezo wa wataalam wa ndani

Mwezi Octoba pia umeaswa kutumika vizuri ili kuweza kuhakiki uelewa wa maswala ya usalama mitandao kwa watumiaji umeweza kufanyiwa kazi huku pakiainishwa jitihada mbali mbali za serikali ya Tanzania inayo endelea nazo kuweza kukabiliana na wimbi la uhalifu Mtandao nchini humo .

TUKAJIKUMBUSHA MATUKIO MUHIMU MATANO YA KIUHALIFU MTANDAO YALIYOJIRI MWAKA HUU.

Huku mataifa mbali mbali yakiendelea kujipanga katika mapambano dhidi ya uhalifu mtandao, bado matukio ya kiuhalifu mtandao yameendelea kuitikisa dunia.

NEIMAN MARCUS

Mwezi wa pili mwaka huu wa 2014, Kampuni ya Neiman Markus ilitengeneza vichwa vya habari baada ya kuingiliwa na wadukuzi wa mitandao waliofanikiwa kuchukua taarifa za wateja wake na kufanikiwa kuzima kila kiashiria ambacho kingeonyesha hali isiyo ya kawaida katika kampuni hiyo.

APPLE

Kampuni ya Apple nayo haikubakishwa salama. Moja ya matukio makubwa yaliyojadiliwa na wana usalama mitandaoni ni pamoja na tukio la wadukuzi mitandao kuingilia, kuchukua na kuzisambaza picha mbaya za watu maarufu kutoka Hollywood ambao walikua wamezihifadhi katika moja ya huduma za Apple maarufu kama iCloud.

Hili halikua tukio zuri kwa Apple pakizingatiwa liliambatana na uzinduzi wa simu zake za iphone 6. Apple walipolizungumzia hili walisema udukuzi ulilengwa moja kwa moja kwa baadhi ya watu maarufu wa Hollywood na si udukuzi wa jumla ambao ungeathiri watumiaji wengi.

TARGET

Wadukuzi mitandao waliingilia kampuni ya taget pia na athari kubwa iliyoikumba kampuni hiyo ambapo udukuzi huo umeigharimu kiasi cha Dola milioni Miamoja na Arobaini na nane za kimarekani.

WAL-MART

Wal-Mart ni moja ya kampuni yenye kuaminika na bahati mbaya wadukuzi walifanikiwa kuingilia na kuiba taarifa ambazo baadae zilipatikana zikisafirishwa kwenda ulaya ya mashariki. Uhalifu huu Wal-Mart walisisitiza kutouzungumzia na mkuu wake wa kitengo cha usalama mitandao kuainisha katika maelezo yake kuwa wanafanya jitihada za dhati kuongeza usalama wa taarifa zake ili kuzuia chochote kinachoweza kuathiri mitandao yake.

HOME DEPOT

Kampuni ya kimarekani ilitengeneza vichwa vya habari baada ya kungundulika wadukuzi mtandao walifanikiwa kuendeleza uhalifu huo kwa miezi mitano hadi walipoweza kugundulika.

Kwa kumalizia, Si vibaya tukaliangalia hili lililozungumziwa Al-hamisi ya tarehe mbili ya mwezi huu wa kumi yakuwa taarifa za majina, namba za simu na mengineyo ya watu zaidi ya Milioni 76 yaliibwa na wadukuzi kutoka katika kampuni ya J.P Morgan Chase. Tukio hili limeelezewa kuwa nitukio kubwa la aina yake